Taarifa..


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo
asubuhi katika Ikulu ya Dar es Salaam
amefanya kikao na Makatibu wakuu,
Manaibu Makatibu wakuu, Gavana wa
Benki Kuu Prof. Benno Ndulu na Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) ili kutoa uelekeo wa Serikali
anayoitaka mara baada ya kuapishwa.
“Nataka Serikali iendelee kwa nguvu zote
na katika kutekeleza dhana ya ‘HAPA KAZI
TU’ na viongozi kuzingatia na kukumbuka
ahadi nilizotoa ili zianze kuonekana na
kufanyiwa kazi mara moja” Rais Magufuli
amesema.
Katika Kikao chake, Rais ametoa
mwongozo na kusisitizia kuwa ni lazima
kila mtendaji Serikalini kuuzingatia,
kufuata sheria na taratibu ili taifa lisonge
mbele kwa ufanisi zaidi.
Katika kikao hicho Rais ameelekeza
mambo kadhaa ambayo watendaji hao
wanapaswa kuyasimamia, kuyawekea
mikakati na kuyapanga vizuri ili atakapo
teua Baraza lake la Mawaziri mambo hayo
yawe tayari ili Mawaziri watakaoteuliwa
waweze kuyasimamia bila kukosa.
Mambo hayo muhimu ni kama ifuatavyo:
Kuanzia mwezi Januari mwaka 2016,
wanafunzi wote wanaoanza shule
watasoma bure bila kulipa ada, Katika
jambo hili, Rais amewataka watendaji
kuanza kuliwekea mikakati tayari kwa
utekelezaji
Suala la mikopo ya wanafunzi nalo
lifanyiwe kazi na mipango yake ikamilike
kwa ajili ya utekelezaji mzuri zaidi
Amefuta safari zote za nje ya nchi kuanzia
leo hadi hapo atakapolitolea suala hilo
maamuzi mengine na kueleza kuwa
shughuli zote zinazotakiwa kufanywa nje
ya nchi zifanywe na kusimamiwa na
mabalozi wa Tanzania wanaowakilisha nchi
huko nje.
Pengine patokee jambo la dharura sana
na hata hilo lazima kibali kitolewe na Rais
au Katibu Mkuu Kiongozi. Badala yake
Rais amewataka watendaji hao kufanya
zaidi ziara za kwenda vijijini ili kuzijua na
kutatua kero za wananchi wa Tanzania.
Katika Kikao hicho, Rais amemtaka
Kamishna wa TRA, Ndugu Rished Bade
kusimamia kwa makini zoezi la ukusanyaji
wa mapato nchini na kuhakikisha kero
ndogo ndogo kwa wananchi lianze
kutekelezwa kama alivyo ahidi kwa
kufanyiwa kazi mapema zaidi.
Rais ameitaka TRA kukusanya mapato
hayo kutoka kwa wafanya biashara
wakubwa zaidi na wale wanaokwepa kodi
bila kuogopa mtu wala taasisi yoyote hapa
Tanzania na kusisitiza kuwa katika Serikali
hii wa kutoa maamuzi vinginevyo zaidi ya
haya ni yeye Rais ama Makamu wake.
Rais Magufuli pia ameagiza usimamizi
katika suala la manunuzi ambalo limekuwa
likitumika vibaya na kuwa mwanya wa
kuibia Serikali kwa watu kuongeza bei ya
vitu hata kama ni vya bei ndogo kabisa
katika jamii.
“Ikitokea suala hilo likagundulika kwa
watu kuongeza bei ya vitu, watendaji
watawajibishwa mara moja”. Rais
amesema, na kuwataka watendaji hao
kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria na
taratibu zilizopo na kuzingatia maadili
mema ya kazi.
………………………MWISHO……………………
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
7 Novemba, 2015 

Post a Comment

Previous Post Next Post