Madawa ya kulevya

MADAWA YA KULEVYA HAYAKUBALIKI VYUONI

Madawa ya kulevya ni kilevya chochote kinachoweza kufifisha uwezo wa kufikiri, uwezo wa kupambanua na kuona mambo, uwezo wa mwili kujikinga na maradhi na mengineo...ni hatari sana kwa mustakabali wa maisha yako, usitumie!
Kwa hapa kwetu Tanzania kuna madawa ya kulevya tuliyozoea kuyaskia kama vile..

1. *Bange na Gundi*
2. *Shisha na ugoro*
3. *Mirungi/Miraa*
4. *Heroine na Cocaine*
Na mengineyo mengi ambayo hutumiwa kwa kuvuta au kujidunga sindano mwilini. Duniani kote matumizi ya dawa za kulevya kwa namna yeyote ile hayakubaliki na serikali za dunia( Ikiwepo ya Tanzania),  taasisi za kidini na za kiraia na vyombo mbalimbali zimekuwa zikipiga kelele usiku na mchana kukataza matumizi ya dawa za kulevya kwani madhara yake huathiri mtu mmoja na kisha jamii nzima kwani tunaishi kwa kutegemeana duniani!

Katika vyuo vikuu wanafunzi pia wamekuwa miongoni mwa watumiaji na wasambazaji wa dawa za kulevya ili hali jamii inawategemea wao kutumia elimu yao na usomi wao kukomboa jamii zetu na kuleta ustawi bora haswa kwa nchi za dunia ya tatu ikiwemo Tanzania. Sasa kama wasomi wa elimu ya juu tunatumika kuuza/kusambaza na matumizi ya  dawa za kulevya, nani atasimama kulikomboa taifa letu na jamii zetu kutoka katika dimbwi la umaskini??

Tumeshuhudia kaka zetu, dada zetu, rafiki zetu, wanafunzi wenzetu wengi wakishindwa kuendelea na masomo yao vyuoni kutokana na matumizi ya dawa za kulevya simply kwa

1.Kukosa uelewa sahihi wa madhara yatokanayo na madawa haya

2. Kuishi kwa kufuata mkumbo, ulimbukeni wa mambo na kutamani vitu vya thamani na anasa au maisha fulani ilihali hauna uwezo nayo

3. Shinikizo la marafiki wanaokuzunguka.

4.Ulaghai wa kifedha toka kwa wafanya biashara hii na mengineyo mengi yanayowasukuma wanafunzi wa elimu ya juu kujihusisha katika biashara hii haramu na matumizi ya madawa haya dhalimu kwa taifa letu, kwa jamii yetu na kwa dunia hii tuliopewa na Mwenyenzi Mungu.

*Chonde! *Chonde* *Chonde* ewe ndugu yangu msomi wa elimu ya juu; matumizi ya dawa za kulevya hayakubaliki na yana madhara makubwa kama haya
1. *Huathiri mfumo wa ubongo kufikiri na udumaza akili*

2. *Huathiri mfumo wa chakula/digestion system na hupunguza na kuondoa hamu ya kula(mfano mirungi)*

3. *Huathiri mfumo wa uzazi / reproduction system(rejea mateja na watumia wa dawa za kulevya hupoteza hamu ya tendo la ndoa na kuzaa)*

4. *Husababisha magonjwa mfano. Tuberculosis (TB), magonjwa ya ngozi na mengineo mengi*

5. *Huathiri mwanadamu kisaikolojia na kimwili ( psychological and physiological problems) rejea mateja na watumiaji wa dawa za kulevya ona miili yao na uwezo wao wa kisaikolojia*

6. *Huathiri jamii kiuchumi, kijamii na namna zote kwani ukishakuwa teja au mtumiaji wa dawa hizi basi unaumiza wazazi,  ndugu na hata wategemezi wako*

6. *Hurudisha maendeleo ya taifa na jamii nyuma kiuchumi, kisiasa na kijamii na taifa laweza kuishia kuwa na raia mazezeta na wagonjwa hivyo litabaki kuwa maskini milele maana hakuna nguvu kazi ya kuzalisha na kulipa kodi kwa maendeleo yetu*

*WITO*
Kwanza waraka huu uwafikie wanafunzi wote wa elimu ya juu na wasomi ukianzia katika chuo kikuu cha Dar es Salaam (kama chuo mama na chuo cha taifa hili) na uwaendee wasomi wa elimu ya juu popote walipo Tanzania na Africa kwamba biashara na matumizi ya dawa za kulevya HAYAKUBALIKI NA TUYAPIGIE KELELE bila kujali changamoto zitazotukabili kama wasomi na watu ambao taifa linatutegemea

Pili, nitoe rai yangu kwa viongozi wa kitaifa, viongozi wa kidini na asasi za kiraia na kila RAIA mwenye akili timamu kwa nafasi yake aunge mkono kampeni/vita hii ya kupinga biashara na matumizi ya dawa za kulevya ili tuweze kulinusuru taifa letu sasa na vizazi vijazo kutoka katika madhara yatokanayo na matumizi ya madawa ya kulevya

Tatu, elimu itolewe kwa njia zote kwenye TV programs, radio, social media, makongamano na warsha na popote penye mikusanyiko ya watu mfano miskitini, makanisani ama iitishwe mijadala kutoa elimu kwa RAIA juu ya madhara makubwa yatokanayo na matumizi ya dawa hizi dhalimu kwa taifa letu na watoto wetu

NNE, wito kwa wanafunzi wenzangu wa elimu ya juu nikianzia na chuoni kwangu Udsm, tusikubali kuwa punda na kutumika vibaya kuwezesha biashara hii haramu ndani ya chuo chetu kwani wanaoathirika ni ndugu zetu, rafiki zetu na hata wasaka madesa wenzetu na wakishatumbukia na kuumia na madawa haya basi inakuwa ndio mwisho wa safari yao kupata elimu kwani hupoteza reasoning ability, performance hushuka na hupelekea Ku disco na kuondolewa chuoni( as a result psychological problems zinaanzia hapo na hatimae tunapoteza watu muhimu kwa taifa hili).

Tano, kumbuka ulipotoka, nini kimekuleta chuo na namna ambavyo wazazi wako wamejinyima na kukulipia ada hadi leo umefika chuo kikuu kisha urudi nyumbani ukiwa teja? Ukiwa zezeta? Ukiwa na GPA dhaifu? Upate discontinuation kwa madawa ya kulevya? Kumbuka ulikuja Mwenyewe usiruhusu marafiki wenye tabia mbaya wakaathiri tabia yako in negative way, simamia msimamo yako na ushike sana dini na uwe na ndoto kubwa za kupata first class GPA, epuka mabashi yasiyokuwa ya lazima sana na epuka ushiriki wako kwa namna yeyote katika biashara na matumizi ya dawa za kulevya kwani sheria na team ya Makonda watakukamata tu

*Mwisho*
*Tuungane na Rais wetu Mh.Dr JPM, Tuungane na mkuu wetu wa mkoa Dar  Mh.Makonda na viongozi wote wa kitaifa kusema
HAPANA KWA BIASHARA NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA* hatimae tutaweza kuinusuru nchi yetu na janga hili la madawa ya Kulevya


Imeandaliwa na
*Tony Mafie*
*Udsm Student*

Post a Comment

Previous Post Next Post