Header Ads

Header ADS

ORODHA YA PILI WANUFAIKA MIKOPO YA ELIMU YA JUU 2024/2025

            ORODHA YA KWANZA YA WANUFAIKA 2024/2025 YATANGAZWA 

Ni awamu ya kwanza yenye wanafunzi 21,509

Mikopo yao ina thamani ya TZS 70.78 bilioni

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo Jumamosi (Septemba 28, 2024) imeanza kutangaza orodha ya wanafunzi wenye sifa waliopangiwa mikopo kwa ajili ya mwaka wa masomo 2024/2025. Awamu hii ya kwanza inajumuisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo ya Shahada ya awali, Shule ya Sheria kwa Vitendo na Shahada ya Uzamili.

Wanafunzi kupata taarifa kupitia SIPA

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Dkt. Bill Kiwia amesema wanafunzi wote walioomba mikopo kwa mwaka 2024/2025 wanaweza kupata taarifa za kina kuhusu mikopo yao kupitia akaunti walizotumia kuombea mikopo maarufu kama ‘SIPA’ - Student’s Individual Permanent Account.

“Leo tumeanza kutoa taarifa za mikopo kwa makundi yote, waliopangiwa mikopo, wapo ambao bado tunaendelea kufanyia kazi maombi yao … kila mwombaji anapata taarifa yake kwenye akaunti ile ile aliyotumia kuombea mkopo, huhitaji kufika ofisi za HESLB”, amesema Dkt. Kiwia na kuongeza kuwa upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wa stashahada na shahada ya Uzamivu unaendelea.

Dkt. Kiwia amesema HESLB imeanza kuandaa malipo ya wanafunzi wapya na wanaoendelea na masomo ambao ni wanufaika wa mikopo na kusema lengo ni kuhakikisha fedha zinafika vyuoni kwa wakati.

245,799 kunufaika na mikopo 2024/2025

“Mwaka huu, Serikali imetenga TZS 787 bilioni kwa ajili ya jumla ya wanafunzi 245,799 wakiwemo zaidi ya wanafunzi 88,000 wa mwaka wa kwanza waliotengewa TZS 284.8 bilioni,’ amesema Dkt. Kiwia na kuongeza kuwa bajeti ya mwaka 2024/2025 imeongezeka kwa TZS 38 bilioni sawa na asilimia 5.1 ikilinganishwa na bajeti ya 2023/2024 iliyokuwa TZS 749.4 bilioni. Mwaka huu pia kiwango cha chini cha mkopo kwa mnufaika  mmoja mmoja kimepanda hadi TZS 3.0 milioni kutoka TZS 2.7 milioni[ME1]  mwaka uliopita wa 2023/2024.

Wito: Vyuo kuwasilisha matokeo ya mitihani

Kuhusu wajibu wa vyuo, Dkt. Kiwia amevikumbusha vyuo ambavyo havijawasilisha matokeo ya mitihani ya wanafunzi-wanufaika wanaoendelea na masomo, kuwasilisha ili kuiwezesha HESLB kuandaa malipo kwa wakati.

“Kuna vyuo vichache, ambavyo bado havijawasilisha matokeo, tumewakumbusha na tunasisitiza waharakishe kuwasilisha matokeo ili tukamilishe malipo ya wanafunzi waliofaulu kuendelea na masomo,” amesema Dkt. Kiwia.

Kuhusu kutangazwa kwa orodha ya Awamu ya Pili

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB amesema kuwa awamu ya pili ya orodha ya wanafunzi waliopangiwa mikopo kwa mwaka 2024/2025 itatangazwa wiki ijayo.

orodha ya pili

HESLB YATANGAZA ORODHA YA PILI WANUFAIKA 2024/2025

Wanafunzi wa shahada mwaka wa kwanza 30,311  

Wanufaika 2,157 mikopo ya ‘Diploma’

Wanafunzi 588 kunufaika na ‘Samia Scholarship’

TZS 99.7 bilioni kutumika kuwagharimia mikopo, ruzuku TZS 2.9 bilioni

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo Jumatano (Oktoba 09, 2024) imetangaza awamu ya pili ya orodha ya wanafunzi wenye sifa waliopangiwa mikopo na ruzuku kwa ajili ya mwaka wa masomo 2024/2025.

Makundi ya walionufaika katika Awamu ya Pili

Orodha iliyotangazwa leo inajumuisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliodahiliwa katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu na vyuo vya kati waliopangiwa mikopo kwa ajili ya Shahada ya awali (30,311) yenye thamani ya TZS 93.7 bilioni. Orodha ya awamu ya pili inafanya idadi ya jumla ya wanafunzi 51,645 waliopangiwa mikopo katika awamu ya kwanza na awamu ya pili kwa ajili ya kugharimia masomo yao ya shahada ya awali ikiwa na thamani ya TZS 163.8 bilioni. Kati ya wanafunzi hao, wanafunzi wa kike ni 22,216 (sawa na 43%) na wa kiume 29,429 (sawa na 57%)

Awamu hii ya pii inajumuisha pia mikopo ya Stashahada (Diploma) kwa wanafunzi wapatao 2,157 yenye thamani ya TZS 5.6 bilioni. Wanafunzi wengine 45 ni wa shahada ya uzamili waliopangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 205.6 milioni na wanufaika 16 wa Shahada ya Uzamivu waliopangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 215.6 milioni.

Kuhusu kutangazwa kwa orodha ya Awamu ya Tatu

HESLB inaendelea kupokea taarifa za udahili kuwezesha kupanga mikopo na kutangaza Awamu ya tatu ya orodha ya wanafunzi waliopangiwa mikopo kwa mwaka 2024/2025 itakayotangazwa siku chache zijazo ili kuwawezesha wanafunzi waliopangiwa mikopo kuendelea na taratibu za kujisajii katika vyuo walikodahiliwa.

Samia Scholarship

Taarifa hii pia ina idadi ya wanafunzi 588 wa shahada ya awali watakaonufaika na fursa za ‘Samia Scholarships’ kwa mwaka huu 2024/2025, ambao wamepangiwa ruzuku yenye thamani ya TZS 2.9 bilioni. Wanafunzi hawa ni wenye ufaulu wa juu katika tahasusi za sayansi na waliodahiliwa katika vyuo mbalimbali kwenye fani za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na hisabati na sayansi za Tiba.

Wito

HESLB inawakumbusha waombaji wa mikopo na ruzuku wenye sifa kwa mwaka 2024/2025 ambao bado hawajapangiwa mikopo au ruzuku, kuendelea kufuatilia taarifa za maombi yao kupitia ‘SIPA’ wakati taratibu za uchambuzi na upangaji wa mikopo na ruzuku zikiendelea.

No comments

Powered by Blogger.