Header Ads

Header ADS

Ratiba ya Mtihani Darasa la Nne 2024

 

RATIBA YA MTIHANI DARASA LA NNE 2024

MAELEKEZO MUHIMU

 1. Hakikisha kuwa unayo Ratiba ya Upimaji wa mwaka 2024 iliyoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania. 

2. Hakikisha kwamba unasoma jina la somo juu ya bahasha husika na kuthibitisha kuwa somo hilo ndilo linalostahili kufanyika wakati huo kulingana na Ratiba ya Upimaji.

 3. Kabla ya kufungua bahasha, mpe Mwanafunzi asome kwa sauti jina la somo lililoandikwa juu ya bahasha ili kuthibitisha ni somo husika kwa mujibu wa ratiba. 

4. Endapo utata utajitokeza kati ya maelekezo yaliyomo katika Karatasi ya Upimaji na Ratiba ya Upimaji, maelekezo yaliyomo katika karatasi ya upimaji husika ndiyo yatakayofuatwa. 

5. Wanafunzi wenye mahitaji Maalum (Wasioona, Uoni hafifu, Viziwi) waongezewe MUDA WA ZIADA WA DAKIKA 20 KWA KILA SAA kwa somo la Hisabati na DAKIKA 10 KWA KILA SAA kwa masomo mengine. 

6. Wanafunzi wenye UONI HAFIFU wapewe karatasi za upimaji zenye maandishi yaliyokuzwa, zilizoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania kwa matumizi yao. 

7. Wanafunzi waelekezwe; 

(a) Kuingia ndani ya chumba cha Upimaji nusu saa kabla ya muda wa Upimaji na watakaochelewa kwa zaidi ya nusu saa baada ya Upimaji kuanza hawataruhusiwa. 

(b) Kufuata maelekezo yote yatakayotolewa na wasimamizi wa Upimaji.

 (c) Kuandika jina kamili na namba ya Upimaji kwa usahihi. 

(d) Kutofanya mawasiliano ya maneno au kwa njia yoyote baina yao. Ikiwa Mwanafunzi ana tatizo anatakiwa kunyoosha mkono ili kuomba msaada kwa msimamizi wa Upimaji. 

(e) Kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu katika Upimaji kwani watakaojihusisha matokeo yao yatafutwa.

 Necta   

ratiba ya mtihani wa Darasa la Nne 2024 PDF

No comments

Powered by Blogger.