Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza rasmi leo tarehe 3 Novemba 2026 matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (Darasa la Saba - PSLE) kwa mwaka 2026.
Ufaulu wa jumla wa wanafunzi umeongezeka, huku takwimu kuu na mifumo ya ufaulu ikionyesha mabadiliko makubwa ikilinganishwa na mwaka uliopita. Taarifa kamili ya matokeo ya shule zote nchini inapatikana moja kwa moja kupitia Tovuti Rasmi ya NECTA.
Takwimu Kuu za Ufaulu Kitaifa (PSLE 2026)
Katika matokeo yaliyotangazwa na Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Said Mohamed, hali ya ufaulu iko kama ifuatavyo:
- Idadi ya Waliofaulu: Wanafunzi 970,876 wamefaulu kwa kupata madaraja ya A, B, na C.
- Asilimia ya Ufaulu: Ufaulu wa jumla ni 85.22% ya watahiniwa 1,139,273 wenye matokeo.
- Ongezeko la Ufaulu: Kuna ongezeko la ufaulu kwa asilimia 3.42 ikilinganishwa na mwaka 2025, ambapo ufaulu ulikuwa asilimia 81.80.
- Ubora wa Ufaulu (Daraja A na B): Jumla ya wanafunzi 429,667 (sawa na 37.72%) wamepata madaraja ya juu ya A na B, ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.82 kutoka mwaka jana
- Kuangalia matokeo y Darasa la saba 2026,Bonyeza kiunganishi hiki hapa chini;