WAZANZIBARI wamesherehekea miaka 52 ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka
1964, ambayo yaling’oa utawala wa Sultani kutoka Oman na kuwezesha
wazalendo wengi kushika hatamu ya kuongoza nchi.
Katika kilele cha sherehe hizi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein atahutubia taifa katika uwanja wa
Amaan.
Matukio mengine makubwa yaliyofanyika katika uwanja huu ni Rais Shein
kukagua gwaride la heshima la vikosi ya ulinzi na usalama, vikiongozwa
na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Amepokea maandamano ya wananchi
wa mikoa mitano ya Unguja.
Rais John Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Makamu wa Rais Mama
Samia Suluhu na Viongozi wastaafu, Mzee Mwinyi, Benjamin Mkapa Aman
Karume na Wengine Wengi wa Kitaifa, wamewasili uwanja wa Amani katika
sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi ya Z'bar.
Vilevile Mkuu wa Majeshi Mwamnyange amehudhulia. Viongozi wengi wa Kitaifa wamehudhulia.
No comments
Post a Comment