UEFA LEO USIKU PSG VS BARCELONA HUKU BENIFICA VS DORTMUND


 UEFA LEO USIKU PSG VS BARCELONA HUKU BENIFICA VS DORTMUND


Michezo miwili ya michuano ya kombe la klabu bingwa ulaya katika hatua ya kumi na sita bora itachezwa leo nchini Ureno na Ufaransa.
Huko nchini Ureno Benfica watakua wenyeji wa Borussia Dortmund kutoka nchini ujerumani mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Sport Lisboa e Benfica, na mwamuzi wa mchezo huo ni Nicola Rizzoli raia wa Italia.
Mchezo wa pili utawakutanisha Paris Saint Germain ya Ufaransa watakaokipiga na miamba wa Hispania Barcelona mchezo ukichezwa katika dimba la Parc des Princes Jijini Paris.

Champions League - Round of 16 February 14
22:45 Benfica vs Borussia Dortmund
22:45 Paris Saint Germain vs Barcelona

Jumatano zitachezwa mechi nyingine mbili Bayern Munich watachuana Arsenal na Real Madrid watatunishina misuli na Napoli ya Italia.
Mechi nyingine nne za michuano hii ya ulaya zitachezwa wiki ijayo

Post a Comment

Previous Post Next Post