Kuongezwa kwa muda wa uhakiki wa wanafunzi wanaotegemea kwenda vyuo.
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)
TAARIFA KWA UMMA
TAARIFA
KWA UMMA KUHUSU KUONGEZWA KWA MUDA WA MAOMBI KWA AJILI YA UHAKIKI WA
TUZO MBALIMBALI KWA WALE WANAOKUSUDIA KUOMBA KUJIENDELEZA KATIKA NGAZI
YA SHAHADA KATIKA VYUO VYA ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018
Baraza la
Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwafahamisha wahitimu wa
Stashahada wanaotaka kujiendeleza katika ngazi ya Shahada kuwa muda wa
kufanya maombi ya uhakiki wa tuzo zao umeongezwa hadi tarehe 15 Agosti
2017.
Hivyo kwa
wale ambao hawakufanikiwa kumaliza maombi ya uhakiki na wale ambao
hawajaomba na wana nia ya kufanya hivyo, sasa wataweza kufanya uhakiki.
Baraza
linapenda kutoa rai kwa waombaji kufanya uhakiki wa tuzo zao mapema ili
kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza katika dakika za mwisho wa muda wa
uhakiki.
Hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya Tarehe tajwa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 19/07/2017
No comments
Post a Comment