Spika ndugai ajiuzulu uspika
Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai amejiuzulu wadhifa wake jana Alhamisi tarehe 6 Januari 2022.
Kwa mujibu wa barua aliyomuandikia Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema uamuzi huo wa kuachia nafasi hiyo ameufanya kwa hiari.
"Naomba kutoa taarifa kwa umma wa Watanzania kuwa jana Tarehe 06 Januari 2022 nimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu nafasi ya Spika wa bunge la Jamhuri .." imesema sehemu ya taarifa hiyo nakuongeza;
"Pia nakala yangu hiyo ya kujiuzulu nimewasilisha kwa katibu wa Bunge kwa ajili ya hatua stahiki kwa mujibu wa katiba ya nchi na sheria nyingine" amesema Ndugai kwenye taarifa yake kwa umma.
Ndugai ambaye ni mbunge wa Kongwa amesema anawashukuru wabunge, Rais Samia Suluhu Hassan, Serikali, wananchi wa Jimbo la Kongwa na Watanzania wote kwa ushirikiano waliompa kipindi akiwa Spika
No comments
Post a Comment