Zitto aongoza wagombea ubunge ACT-Wazalendo
CHAMA cha ACT Maendeleo kimetoa rasmi majina ya wagombea wake watakaokiwakilisha chama hicho, katika nafasi za ubunge na uwakilishi kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, huku Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Kabwe Zitto akiwania ubunge jimbo la Kigoma mjini.
Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho kwa vyombo vya habaeri, pamoja na Zitto pia kimewateua wabunge wengine waliokuwemo kwenye Bunge lililopita ambao ni Moses Machali, anayewania jimbo la Kasulu Mjini, Anna Mallack Mpanda vijijini na Chiku Abwao Iringa Mjini.
Machali katika Bunge lililopita alikuwa mbunge wa Kasulu mjini kupitia NCCR-Mageuzi wakati Mallack na Abwao walikuwa wabunge wa viti maalum kupitia Chadema, wabunge wote hao wamehama vyama hivyo na kujiunga na chama hicho cha ACT.
Wagombea wengine waliopitishwa na chama hicho kukiwakilisha katika nafasi ya ubunge ni Eva Kaka (Bahi), Christina Kamunya (Dodoma Mjini), Said Njuki (Kondoa), Demi Mchuki (Kondoa Mjini) na Fataha Ibrahim (Kondoa Kusini).
Baadhi ya wagombea wengine ni Maulid Mataka (Kongwa), Batulo Ibrahim (Arumeru Mashariki), Estomih Mallah (Arusha Mjini), Alex Kisanga (Karatu), Ojung Saitabau (Arumeru Magharibi), Geovan Meleki (Rombo), Fadhili Fadhili (Mwanga) na Lilian Mduma (Same Magharibi).
Aidha chama hicho pia kimemteua Hassan Rashid kuwania jimbo la Same Mashariki, Goodluck Mollel (Moshi Vijijini), Nuru Mohammed (Hai), Buni Ramole (Moshi Mjini), Msumba Mngumi (Mlalo), Ally Tendeza (Mkinga), Mikidadi Hamisi (Bumbuli) na Zaina Bongi (Korogwe Vijijini).
Katika jimbo la Korogwe Mjini chama hicho kimemteua Mohammed Mwalimu kuwania nafasi hiyo, Zuberi Ngoda (Muheza), Ahmad Kidege (Tanga Mjini), Bakari Mrisho (Handeni Vijijini), Ramadhani Mwalekwa (Handeni Vijijini), Charles Mtuu (Handeni Mjini) na Onesmo Mwakyombo (Mikumi).
Jimbo la Morogoro Kusini chama hicho kimemteua Hamimu Muhongo kuwania nafasi hiyo, Jafari Chamkua (Morogoro Kusini Mashariki), Isaya Maputa (Ulanga Mashariki), Selemani Msindi (Morogoro Mjini), Athuman Adam (Mvomero) na Hidaya Sanga (Malinyi).
Wengine ni Mwinyi Madega (Gairo), Hassan Mbaruku (Kilosa Kati), Saidi Saidi (Bagamoyo), Gasper Shoo (Chalinze), Rose Mkonyi (Kibaha Vijijini), Mohammed Massaga (Kisarawe), Kunje Ngombale-Mwiru (Mkuranga), Habibu Amiri (Rufiji) na Ahmad Kigomba (Mafia).
Wagombea wengine wa chama hicho walioteuliwa ni Habibu Mchange (Kibaha Mjini), Janeth Rite (Kawe), Dickson Nghilly (Kibamba), Mohammed Mwikongi (Segerea), Ally Shaabani (Ukonga), Mohammed Ngulangwa (Temeke), DianaRose Joseph (Kigamboni) na Maftah Sudi (Kilwa Kusini).
Aidha jimbo la Nachingwea ACT imemteua Mosha Emmanuel kuwania nafasi hiyo, Pilima Sijaona (Newala Vijijini), Lulindi ni Francis Ngaweje, Mtwara Mjini yupo Bakari Mtila, Tunduru Kusini amesimamishwa na Ally Abdallah, Songea Mjini yupo Emmanuel Ndomba, Namtumbo ameteuliwa Boniface Thawe na katika Jimbo la Madaba yupo Kuhani Loston.
Wagombea wengine ni Raymond Ndomba (Nyasa), Mwanahamisi Mayinga (Kalenga), William Kasika (Isimani), Daniel Mwangili (Mufindi Kaskazini), James Kitime (Mafinga Mjini), Salim Nyemolelo (Mufindi Kusini), Taji Mtuga (Kilolo), Michael Nyilawila (Songwe), Hosea Mwanjoje (Mbeya Vijijini) na Samwel Motto (Kyela).
Pia Frank Magoba aliteuliwa na chama hicho kuwania jimbo la Rungwe, Gwandumi Mwakatobe (Busekelo), Julius Philipo (Mbozi), Rosemary Mwashamba (Vwawa), Lusekelo Asheri (Mbeya Mjini), Lucy Okeyo (Momba), Reddy Makubha (Tunduma), Paul Mbogho (Singida Vijijini), Kapalatu Salim (Manyoni Magharibi) na John Mottee (Manyoni Mashariki).
Jimbo la Singida Mjini anayewania nafasi hiyo kupitia chama hicho ni Anna Mghwira, Joram Ntandu (Singida Magharibi), Devatus Munna (Singida Mashariki), Henry Mollo (Mkalama), John Patrick (Nzega Vijijini), Abdallah Kondo (Nzega Mjini), Peter Kabuya (Bukene), Tito Alex (Igunga), Leopald Mahona (Manonga), Kirungi Kirungi (Kaliua), Msafiri Mtemelwa (Urambo), Godwin Kayoka (Ulyankulu), Kansa Mbarouk (Tabora Kaskazini) na Bakari Mtongwa (Igalula).
Kwa upande wa Zanzibar chama hicho kimesimamisha wabunge na wawakilishi katika majimbo yote na baadhi ya walioteuliwa kuwania nafasi hizo ni Masoud Suleiman Bakari (Konde), Juma Hamad Juma (Micheweni), Hamad Shehe Tahir (Tumbe) na Mbarouk Ali Khamis (Wingwi).
Wengine ni Suleiman Ali Hassan (Gando), Ali Makame Issa (Kojani), Salim Sheha Salim (Mtambwe), Husna Salim Omar (Mgogoni), Hassan Abdalla Omar (Wete), Asha Bakari Mohammed (Chake), Ridhiwan Khamis Nasib (Chonga) na Ali Salum Humud (Ole).
No comments
Post a Comment