Header Ads

Header ADS

lowasa ajiunga rasmi na chadema


  HABARI HATIMAYE EDWARD LOWASSA
AJIUNGA RASMI CHADEMA NA
AKABIDHIWA KADI
 
Lowassa: Namshukuru mke wangu Regina,
wanangu na wanafamilia katika kipindi hiki
kigumu kilichojitokeza.
Lowassa: Nawashukuru wanaCCM
waliojitokeza kuniunga mkono wakati
nikitafuta wadhamini.
Lowassa: Kilichotokea Dodoma, ni kupora
madarakani ya kamati kuu, waswahili
wanasema kubaka madaraka.
Lowassa: Chuki na roho mbaya zilitawala
licha ya mimi kuwa mgombea mwenye
ushawishi na anayekubali zaidi kuliko wote
Lowassa:Kwa mantiki hii nitakuwa mnafiki
kama nitaendelea kudanganya nafsi yangu
na Watanzania kuwa bado nina imani na
CCM
Lowassa: Sijakurupuka kwa uamuzi huu,
nawaomba watanzania wajiunge na
UKAWA katika Safari ya Matumaini.
Lowassa: Wanaoogopa kisasi wamefanya
madhambi gani? Waulizeni..mimi ni
Mkristo,sina kisasi..waende wakatubu kwa
Mungu wao
Lowassa: CCM Si baba yangu wala Mama
yangu. Watanzania kama wameyakosa
mabadiliko ndani ya CCM, basi watayapata
nje ya CCM.
Lowassa hatimaye amemaliza rasmi
kujiunga na CHADEMA na watu sasa
wanashangilia wakiimba
'Tunaimani na Lowassa,  

No comments

Powered by Blogger.