ORODHA YA MAJINA WANAOTAKIWA KUSAHIHISHA MAOMBI YA MIKOPO 2019/2020

ORODHA YA MAJINA WANAOTAKIWA KUSAHIHISHA MAOMBI YA MIKOPO 2019/2020


HESLB imetoa orodha ya waombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020 ambao fomu zao zina upungufu ili wafanye marekebisho kwa siku nne kuanzia leo Jumatatu ambapo pia mwongozo wa jinsi ya kufanya marekebisho utatolewa..

Hatua ya HESLB inafuatia kukamilika kwa uhakiki wa maombi ya mikopo ambapo imebainika baadhi ya fomu za maombi ya mikopo zina upungufu unaozuia kuendelea na hatua ya kupangiwa mikopo.

Upungufu huo ni pamoja na kukosa nyaraka ama viambatanisho vilivyothibitishwa na mamlaka husika na saini za waombaji na wadhamini wao.

Orodha hii ni ya wanafunzi wanaokwenda kusoma masomo ya Shahada ya kwanza. Orodha ya waombaji mikopo watakaojiunga na Shule ya Sheria (Law School of Tanzania), Shahada za Uzamili na Uzamivu

Ili kuona orodha ya majina na marekebisho yanayohitajika *bofya hapa.*

Post a Comment

Previous Post Next Post