Header Ads

Header ADS

Tanzia Tanzia Mh.Benjamin mkapa atunae tena ametutoka leo,mungu ailaze pema p

Raisi mstaafu Benjamin Mkapa  anatarajiwa kuzikwa Jumatano tarehe 29 mwezi huu kijijini kwake Lupaso mkoani Mtwara

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuanzia siku ya Jumapili, Watanzania wote watapata fursa ya kushiriki shughuli za kuaga zitakazofanyika katika uwanja wa uhuru jijini Dar es Salaam.
Shughuli za kumuaga mzee Mkapa zitafanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 26 mpaka tarehe 28, kuanzia Jumapili mpaka Jumanne.
Siku ya Jumapili kuanzia saa nne asubuhi, Kanisa Katoliki litaongoza misa ambayo wakazi wa Dar es Salaam na nje ya mji huo watapata fursa ya kuaga mwili baada ya misa na zoezi hilo litaendelea siku nzima mpaka siku ya Jumatatu siku nzima pia itatumika kwa shughuli hiyo.
Waziri Majaliwa amesema siku ya Jumanne tarehe 28 itakuwa siku ya kuaga kitaifa ambapo viongozi mbalimbali wa serikali nchini , viongozi wa dini, na wananchi.
Baada ya zoezi hilo majira ya alasiri mwili wa Kiongozi mstaafu wa taifa hilo utasafirishwa kwenda wilayani Masasi.
Mwili wa marehemu utatua katika uwanja wa ndege wa Nachingwea na kutoa fursa kwa wakazi wa eneo hilo kuaga mwili wa marehemu.

No comments

Powered by Blogger.