Tuzo za VPL 2020


Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) Tanzania Bara, ziliuzuliwa na Mgeni rasmi  ambaye alikuwa  Waziri wa TAMISEMI, Suleiman Jaffo akiwa pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia kwa ajili ya utoaji wa tuzo hizo jana  Agosti 7, 2020. 
Tuzo zilitolewa kwa wachezaji, makocha na waamuzi bora wa ligi hiyo katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Hii ndiyo orodha ya washindi wa tuzo hizo.
Tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu na kiasi cha hundi ya Fedha (10,000,000) imechukuliwa na Meddy Kagere, na kupokelewa na Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu. 


Mshindi wa kwanza wa Ligi Kuu Vodacom ambayo Klabu ya Simba wamelamba zawadi ya Milioni Mia Moja

Mshindi wa pili ni Klabu ya Yanga wao wamepata zawadi ya Shilingi milioni 45
Mshindi wa Tatu ni Azam Fc ambao wao wamepata zawadi ya Shilingi milioni 30.
Washindi wa Nne ni timu ya Namungo wao wamepata zawadi ya Shilingi milioni  Kumi.

Tuzo ya mchezaji bora chipukizi imekwenda kwa Novatus Dismas wa Biashara United akiwashinda Kelvin Kijiri wa KMC na Dickson Job wa Mtibwa Sugar.

Tuzo ya kocha bora imekwenda kwa Sven Vandenbroeck wa Simba akiwashinda Hitimana Thierry wa Namungo FC na Aristica Cioaba wa Azam FC na.

Tuzo ya golikipa bora imekwenda kwa Aishi Manula wa Simba akiwashinda Daniel Mgore wa Biashara United na Nouridine Balora wa namungo FC.

Ramadhan Kayoko wa Dar es Salaam ndiye mwamuzi bora wa msimu akiwapiku Ahmed Arajiga wa Manyara na Abdallah Mwinyimkuu wa Singida.

Nico Wadada kutoka Azam FC ndiye beki bora wa msimu, akiwapiga chini David Luhende wa Kagera Sugar na Bakari Mwamnyeto kutoka Coastal Union.

Clatous Chama kutoka Simba SC ndiye mchezaji bora wa msimu akiwashinda Bakari Mwamnyeto wa Coastal Union na Nico Wadada wa Azam FC.

Tuzo ya mwamuzi bora msaidizi imekwenda kwa Frank Kombe wa Dar es Salaam akiwapiku Abdulaziz Ally wa Arusha na Hamdan Said wa Mtwara.

Tuzo ya kiungo bora imekwenda kwa Clatous Chama wa Simba SC akiwashinda Lucas Kikoti wa Namungo FC na Mapinduzi Balama wa Yanga.

Timu yenye nidhamu bora msimu wa Ligi Kuu 2019/2020 imechukuliwa na Kagera Sugar.

TUZO YA HESHIMA: Tuzo hii imetolewa kwa Sunday Manara ‘Computer’, ambaye amekabidhiwa hundi ya Sh Milioni 3 kutokana na kuwa Mchezaji wa Kwanza kutoka Tanzania kucheza Barani Ulaya

Post a Comment

Previous Post Next Post