TAMKO RASMI LA BALOZI JUMA V. MWAPACHU.


TAMKO RASMI LA BALOZI JUMA V. MWAPACHU. NAJIVUA UANACHAMA WA CCM

Ndugu zangu,
Kesho ni siku muhimu katika kalenda ya Taifa
letu. Tunamkumbuka marehemu Baba wa Taifa,
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyetutoka
miaka 16 iliyopita. Nadhani ni siku mwafaka
kwangu kufanya maamuzi magumu katika
maisha yangu ambayo yanahusu uanasiasa
wangu. Mimi ni mwanachama wa CCM tangu
mwaka 1967 wakati nilipojiunga na TANU
Youth League. Nimepata fursa ya kuwa
kiongozi ndani ya Chama hiki. Lakini kuanzia
kesho mimi si mwanachama wa CCM tena.
Natoa maelezo yafuatayo:
Kwa kipindi chapata mwezi na nusu hivi sasa
mmekuwa mkisoma makala zangu kuhusu
msimamo na mwelekeo wangu katika masuala
ya siasa za hapa nchini hususan kuhusu
uchaguzi mkuu na mstakabali wa demokrasia
nchini mwetu. Nyote mnatambua kwamba
kuanzia mchakato wa kumpata mgombe wa
Urais ndani ya CCM kule Dodoma, ambako
nilipiga kambi, sijayumba katika msimamo
wangu kwamba Edward Ngoyai Lowassa ndiye
chaguo langu katika kampeni za kumpata Rais
mpya wa Taifa letu.
Chaguo langu si ndoto wala mlipuko wa
mapenzi juu ya Lowassa.
Nimemfahamu Lowassa tangu miaka ya 90
nikiwa cadre wa Chama cha Mapinduzi kwa
mahusisho katika majukumu ya Kic,ssa amejaaliwa nuru na uwezo wa
kuongoza na wa kupendwa na watu. Ni msikivu
pamoja na kwamba ni kiongozi asiyependa
ukiritimba na utovu wa nidhamu, iwe kwa
upande wa watumishi au wananchi wenyewe.
Kubwa kwake ni ucha Mungu wake ambao
unamsaidia sana katika uongozi unaojali na
kuheshimu utu, ukweli na uwazi. Wanaodhani
au kutaharuki kwamba eti anaweza au ana
hulka ya kulipiza kisasi kwa jambo lolote lile ni
waongo; wanajilinda.
Lowassa ni chaguo la wengi na CCM, katika
busara yake ya kumuengua katika mchakato wa
kumpata mgombea wa Urais, kimedhihirisha
kutokuwa Chama kinachoendeshwa kwa misingi
ya demokrasia. Dalili za Chama hiki kupoteza
lengo la kuwa Chama cha watu, na kuwa cha
viongozi wachache zilianza siku nyingi na hasa
katika kipindi cha uongozi wa Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete. CCM kimebadilika na
kuwa Chama cha makundi na migawanyiko
yakupambana, si kwa malengo ya itikadi na
ujenzi wa Chama, bali ya kumalizana na kutaka
kufukuzana.
Lowassa angeweza kufukuzwa miaka mingi tu
iliyopita! Aliweza kushinda vita hivyo kutokana
na kupendwa na wengi ndani ya CCM. Hivyo,
kujitoa kwake uanachama wa CCM hivi karibuni
ni sahihi kabisa kwasababu CCM si Chama tena
cha watu. Kimetekwa. Na mimi nakubaliana na
msimamo wa Lowassa na hao waliyofuata
kutoka nadani ya CCM.
Niliwahi kuandika makala katika ukurasa huu
nikimnukuu mshairi mmoja wa Uingereza
aliyeandika kwamba, ‘there comes a time when
the door opens and allows the future in’.
Mlango huo sasa umefunguka usoni mwangu na
huu uamuzi wangu maana yake ni kukubali
kwamba wakati mpya umewadia; ni wakati wa
mabadiliko. Kuendelea kujihisi kwamba ningali
mwana CCM wa kadi ni kukubali kujidanganya
mwenyewe. Si sawa. Kama marehemu Baba wa
Taifa alivyowahi kusema, ‘CCM si mama yangu’.
Hivyo ndugu zangu, kuanzia kesho mimi si
mwana CCM tena. Nitarejesha rasmi kadi yangu
kupitia ofisi ya CCM ya kata yangu Mikocheni,
Dar-es-Salaam. Kwa sasa sijaamua kujiunga na
Chama kingine.
Mwenyezi Mungu anilinde. 

Post a Comment

Previous Post Next Post