Wanafunzi wa vyuo-NEC


 TUME ya taifa ya Uchaguzi sasa imethibitisha
kuwa wanafunzi wa Vyuo vikuu hawatapiga
kura katika uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza katika kipindi cha kikaangoni
kinachorushwa na EATV, jana Emmanuel
Kawishe amesema kuwa wanafunzi hao
hawataweza kupiga kura kuchagua
diwani,mbunge au Rais kwa kuwa sheria
inasema kila mtu atapiga kura pale
alipojiandikishia.
“Sheria ya uchaguzi kifungu cha 61(3)a
kuwa kila aliyejiandikisha atapiga kura
alipojiandikisha” alisema Kawishe.
Aidha amefafanua kuwa vituo vyote vya kupigia
kura vitafunguliwa saa 1 asubuhi na vitafungwa
saa kumi jioni hivyo kuwatahadharisha wapiga
kura wote kuwepo kituoni kabla muda wa
kufunga.
Taarifa ya kutopiga kura kwa wanafunzi wa
vyuo vikuu imekuwa rasmi huku viongozi wa
Wanafunzi vyuo vikuu wakihangaika kupeleka
shauri mahakamani ili serikali ifungue vyuo
kwa wakati na kuwapa wao fursa ya kupiga
kura.
Hii ni mara ya pili kwa Vyuo vikuu kufunguliwa
baada ya Oktoba, kwa mara ya kwanza
ilifanyika vile vile mwaka 2010 kwa kisingizio
cha mikopo ya Elimu ya juu.
Ushahidi kutoka kwa wanafunzi mbalimbali
waliowahi kunufaika na mikopo wanasema
serikali haijawahi kutoa mikopo kwa wakati
licha ya sababu za mara kwa mara kuahirisha
kufungua vyuo wakati wa Uchaguzi.
Mapema mwaka huu, Shirikisho la wanafunzi
wa wanachadema wa Vyuo vikuu (Chaso)
kupitia Kaimu Mratibu wao Wilfred
Mwalusanya aliitaka NEC kueleza utaratibu wa
kuwaandisha wanavyuo ili wakati wa kupiga
kura waweze kushiriki.
Tayari tuhuma zimeanza kutolewa na wadau
mbalimbali kuwa tume imetumiwa na serikali
ya CCM ili kuinusuru sababu wanavyuo
wamehamasika kuelekea uchaguzi mkuu mwaka
huu. 

Post a Comment

Previous Post Next Post